Iran
-
Mousavi: Matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani yanangilia mambo ya ndani ya Iran
Dec 13, 2019 12:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani akisema kuwa matamshi kama hayo yanayoingilia masuala ya ndani ya Iran hayaweza kuficha makosa ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kutotekeleza majukumu yao katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na misimamo yao isiyo sawa kuhusiana na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani.
-
Hatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran alaani njama za maadui dhidi ya Iran
Dec 13, 2019 11:34Hatibu wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesisitiza udharura wa kutatuliwa matatizo ya kimaisha ya wananchi hususan baada ya kupandishwa bei ya mafuta hapa nchini
-
Jahromi: Usafirishaji vifurushi vya Posta Iran, sasa utafanyika kwa kutumia ndege zisizo na rubani
Dec 13, 2019 07:53Mohammad Javad Azari Jahromi, Waziri wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, wizara yake imezindua mfumo wa Posta, ujulikanao kama Post-Plus na kuongeza kuwa, kuanzia sasa usafirishaji wa vifurushi vya posta utafanyika kwa kutumia ndege zisizo na rubani za droni ambazo zina uwezo wa kufika kila pembe ya nchi.
-
Aghalabu ya waliouawa katika ghasia za Iran, hawakuwapo kwenye maandamano
Dec 13, 2019 00:44Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema asilimia 85 ya watu waliouawa katika ghasia za hivi karibuni hapa jijini Tehran hawakuwepo kwenye maandamano au mikusanyiko yoyote, bali walilengwa na watu fulani kwa niaba ya maadui.
-
Nia njema na kuaminiana; mambo ya lazima ya kupatikana usalama wa Ghuba ya Uajemi
Dec 12, 2019 13:34Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiiislamu ya Iran amelaani vikali taarifa ya mwisho ya kikao cha 40 cha wakuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi kilichofanyika huko Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia na kusema kuwa, waungaji mkono wa siasa zisizo na hekima katika eneo hili la Mashariki ya Kati wanapaswa kutoa majibu na kuwajibika mbele ya fikra za waliowengi.
-
Meja Jenerali Salami: Taifa la Iran halitawendea maadui kwa ajili ya kutatua matatizo ya kiuchumi
Dec 12, 2019 12:41Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) amesema kuwa, matatizo yote ya kiuchumi ya Iran yametokana na vikwazo vya kidhalimu vya maadui.
-
Iran: Wanaounga mkono siasa zisizo na hekima katika eneo wanapaswa kuwajibika
Dec 12, 2019 02:18Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali taarifa ya kikao cha 40 cha wakuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi na kusema kuwa, waungaji mkono wa siasa zisizo na hekima katika eneo hili la Mashariki ya Kati wanapaswa kutoa majibu na kuwajibika mbele ya fikra za waliowengi.
-
Rouhani: Njama za Marekani dhidi ya wananchi wa eneo zitagonga mwamba
Dec 11, 2019 12:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa njama za Marekani dhidi ya Iran, Iraq, Syria, Lebanon, Afghanistan, Pakistan, Yemen na nchi nyingine za eneo hili zitafeli kwa kushirikishwa wananchi.
-
UN: Hakuna ushahidi kwamba Iran ilihusika na mashambulizi dhidi ya Aramco, Saudia
Dec 11, 2019 08:04Ripoti iliyotolewa na wachunguzi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa Saudi Arabia imesema kuwa, hawajapata ushahidi wa aina yoyote unaothibitisha kuwa Iran ilihusika na mashambulizi dhidi ya taasisi za mafuta za Saudi Arabia.
-
Iran inapinga kutumiwa haki za binadamu kama chombo cha kisiasa
Dec 11, 2019 01:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametoa jibu kwa taarifa ya Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya na kusema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga kutumiwa haki za binadamu kama chombo cha kisiasa dhidi ya nchi huru na zenye kujitegemea."