Feb 29, 2016 02:35 UTC
  • Maziko ya mtegeneza filamu mashuhuri wa Iran

Maziko ya mtengeneza filamu mashuhuri wa Iran, Farajullah Salahshur yalifanyika jana Jumapili kwa kushiriki idadi kubwa ya wapenzi wa tasnia ya filamu hapa nchini.

Mwana wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Mojtaba Khamenei, naye ameshiriki kwenye maziko hayo.

Kabla ya hapo, Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikuwa ametoa mkono wa pole kwa wafiwa wote kufuatia kifo cha mtengeneza filamu huyo maarufu aliyeshikamana vizuri na mafundishoya dini tukufu ya Kiislamu.

Farajullah Salahshur, ambaye ametengeneza filamu nyingi maarufu kama vile Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf AS na Kisa cha As’habul Kahf aliaga dunia juzi Jumamosi akiwa na umri wa miaka 63. Kabla ya kufariki dunia, Salahshur alikuwa ameshaandika kisa cha filamu ya Maisha ya Nabii Musa AS. Uchukuaji filamu wa kisa hicho ulipangwa kuanza miezi michache iliyopita, lakini hilo halikuwezekana kutokana na ugonjwa ulioishia kwenye kifo chake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amminie rehema Zake na amlaze mahala pema peponi na amfufue pamoja na waja wema.

Tags