May 21, 2018 08:11 UTC
  • Rais Rouhani: Marekani haiwezi kukabiliana na taifa imara la Iran

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kwamba kamwe Marekani haitoweza kulipigisha magoti taifa imara la Iran.

Alisema hayo jana usiku  akiwa pamoja na familia za baraza la mawaziri na wafanyakazi wengine wa serikali yake.

Rais Rouhani aidha ameashiria mashinikizo na njama za uistikbari wa dunia, utawala wa Kizayuni wa Israel na vibaraka wao katika eneo hili za kutaka kutoa pigo kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, taifa la Iran limesimama kidete kukabiliana na mashinikizo yote hayo.

Ramadhani ni mwezi wa ibada na toba. Ni mwezi wa usafi wa moyo, mwili na maeneo. Hapa Waislamu wa Iran wakisafisha kuta za msikiti kuikaribisha Ramadhani

 

Vile vile amesema, taifa kubwa la Iran linaendelea vyema na njia yake liliyojichagulia na litafanikiwa tu kwani Wairani wameamua kujisimamia na kujitegemea wenyewe.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema, mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa rehema, maghufira na wenye baraka nyingi za Mwenyezi Mungu.

Ameongeza kuwa, moja ya athari nzuri za mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kwamba mwezi huu unaleta mapenzi, unazidisha hali ya kushibana na mazingira ya watu kuwa karibu zaidi baina yao.  

Tags