Jun 10, 2018 07:53 UTC
  • Iran: Nchi za Kiislamu zinapaswa kuungana kulihami taifa linalodhulumiwa la Palestina

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uturuki amesema, nchi za Waislamu na mataifa huru duniani yanapaswa kuwa kitu kimoja katika kulihami na kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Shirika la habari la Mehr limemnukuu Mohammad Ebrahim Taherian Fard akisema hayo katika taarifa aliyoitoa kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds na kuongeza kuwa, maadhimisho ya siku hiyo (Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani) ni kumbukumbu nzuri iliyoachwa na Imam Khomeini MA, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni njia bora ya kuleta umoja na kupanua anga ya udugu baina ya Waislamu wa mataifa na madhehebu yote. 

Balozi Mohammad Ebrahim Taherian Fard na Rais Recep Tayyip Erdogan

 

Amesema, kuizingatia kadhia ya Palestina kunaweza kuleta mshikamano mkubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba nafasi ya Iran na Uturuki katika suala hilo ni muhimu sana hasa kwa kuzingatia kuwa nchi hizi mbili za Waislamu zina taathira kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu.

Vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zimekuwa zikfianya juhudi zenye taathira kubwa katika kuwahami ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina kiasi kwamba hata katika kikao cha dharura cha viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kilichofanyika mjini Istanbul, Uturuki, viongozi wote walikubaliana kwa kauli moja kuhusu wajibu wa kupambana na Wazayuni maghasibu.

Balozi huyo wa Iran nchini Uturuuki pia amesema, mbali na Tehran na Ankara kushirikiana katika kuwatumia misaada wananchi madhlumu wa Palestina, ushirikiano wao utalenga pia kuleta maelewano na mshikamano kwa ajili ya kutatua matatizo ya kieneo hususan ya ulimwengu wa Kiislamu.

Tags

Maoni