May 27, 2019 14:46 UTC
  • Iran yataka nchi za Ghuba ya Uajemi ziwe macho kuhusu vitisho vya Marekani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema: "Sera za Marekani za vikwazo dhidi ya Iran zimehatarisha amani na usalama katika eneo hili zima na hivyo nchi za eneo zinapaswa kuwa macho kuhusu vitisho hivyo."

Sayyed Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayesimamia masuala ya kisiasa ameyasema hayo Jumatatu wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Muhammad al Khalid al Ahmad al Sabah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait.

Katika mazungumzo hay yaliyofanyika Kuwait City, mji mkuu wa Kuwait, Araqchi ameashiria sera za kimsingi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu ulazima wa kuwepo amani na utulivu katika eneo muhimu la Ghuba ya Uajemi na kuongeza kuwa usalama unajumuisha pia utulivu katika sekta za kisiasa na kiuchumi.

Sayyed Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akifanya mazungumzo na Muhammad al Khalid al Ahmad al Sabah, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait katika Mji wa Kuwait Mei 27 2019

Araqchi ameashiria sera za uwajibikaji za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu matukio ya eneo hili na kuongeza kuwa: "Mazungumzo na mashauriano na nchi za eneo hili ni kati ya misingi ya sera za kigeni za Iran, na ndio maana Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuanzisha mchakato wa kieneo wa kufanyika mazungumzo yenye manufaa baina ya nchi zote za eneo hili."

Naibu Waziri Mkuu wa Kuwati naye kwa upande wake amemkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini humo na huku akiashiria hali ya hivi sasa katika eneo hili amesisitizia umuhimu wa kuendelea mazungumzo na mashauriano baina ya nchi jirani.

Sayyid Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amewasili leo nchini Kuwait katika fremu ya safari yake ya kuzitembelea nchi za eneo hili la Ghuba ya Uajemi.

Tags