Sep 11, 2019 03:24 UTC
  • Zarif amwambia Trump, kaulimbiu ya Netanyahu ni: Tutapigana vita hadi askari wa mwisho wa Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemtumia ujumbe wa Twitter Rais Donald Trump wa Marekani akisema: Kaulimbiu ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ni: Tutapigana vita hadi atakapobakia askari wa mwisho kabisa wa Marekani.

Muhammad Javad Zarif ametuma mkanda wa video katika mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu na kuandika kuwa: "Trump, hivi unajua kwamba, Netanyahu ndiye aliyeitumbukiza Marekani katika kinamasi cha vita vya Afghanistan? Hicho ni kinamasi ambacho hata wewe  mwenyewe unajua vyema kwamba huwezi kuondoka ndani yake."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amechapicha picha kadhaa kutoka mtandao wa C-SPAN wa Marekkani katika ukurasa wake wa Twitter ambazo zinamuonesha Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu akiihamasisha Marekani kupambana na kile alichokiita kuwa ni tawala na nchi za kigaidi. 

Muhammad Javad Zarif

Mwaka 2001 Marekani na waitifaki wake waliishambulia na kuivamia nchi ya Afghanistan kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, na tangu wakati huo ukosefu wa amani, ugaidi na uzalishaji wa dawa za kulevya vimeongezeka mara dufu nchini Afghanistan. 

Maafisa wa serikali na watu wa Afghanistan wamekuwa wakiandamana mara kwa mara wakitaka kuondoka majeshi vamizi ya Marekani na waitifaki wake nchini humo.      

Tags

Maoni