Sep 18, 2019 12:08 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Matembezi  ya Arubaini yanaendelea kuchukua sura ya kimataifa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, matembezi ya Arubaini yanaendelea kuchukua sura ya kimataifa na kuongeza kuwa: "Ujumbe wa Imam Hussein AS ni wa kuikomboa dunia kutoka katika utawala wa kambi ya ukafiri na uistikbari."

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran katika hafla ya kuwakirimu na kuwashukuru Wairaki kutokana na huduma na ukarimu wao kwa wageni wa matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS. Amesema matembezi hayo ni maudhui isiyo na kifani  na ya kimataifa ambayo inaandaa mazingira ya kuenea maarifa ya Imam Hussein AS na kuundwa na ustaarabu mpya wa Kiislamu. Ameongeza kuwa, Imam Hussein AS si maalumu kwa Mashia pekee bali ni wa madhehebu zote za Kiislamu ziwe ni za Kishia au Kisunni na pia kwa wanaadamu wote na ni kwa msingi huo ndio katika matembezi ya Arubaini pia kuna wasio kuwa Waislamua ambao hushiriki.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: "Iwapo uwezo mkubwa wa mataifa ya Kiislamu katika maeneo ya Asia Magharibi na Afrika Kaskazini utaunganishwa na kubainika kivitendo basi wakati huo tunaweza kuona maana halisi ya izza ya Mwenyezi Mungu na ustaarabu adhimu wa Kiislamu utaweza kuwadhihirikia walimwengu."

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi katika hafla ya kuwakirimu na kuwashukuru Wairaki kutokana na huduma na ukarimu wao kwa wageni wa matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS

Ayatullah Khamenei amesema nyoyo za mataifa mawili ya Iraq zimeungana na kuongeza kuwa: "Maadui wamejaribu sana kuleta mifarakano baina ya mataifa haya mawili lakini, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu hawajaweza kufanikiwa na hawatafanikiwa kwa sababu msingi wa mshikamano wa mataifa ya Iran na Iraq ni  imani kwa Mwenyezi Mungu SWT na Mapenzi kwa Ahlul Bayt AS pamoja na Mapenzi kwa Imam Hussein AS.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amekumbusha kuhusu njama za miaka 40 na visitsho vya Marekani na mamluki wake dhidi ya taifa la Iran na kusema pamoja na kuwepo njama zote hizo, maadui wameambulia patupu kwani Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imestawi kutoka mche mdogo hadi mti wenye matunda  ambayo yanazidi kuenea.

Ayatullah Khamenei ameashiria nara za hadhirina kuhusu kuangamizwa Marekani na utawala wa Kizayuni na kusema: "Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu nara hizo zitaweza kufikiwa katika mustakabali usio mbali na umma wa Kiislamu utapata ushindi mbele ya maadui."

Tags

Maoni