Sep 18, 2019 12:14 UTC
  • Rouhani: Mapambano ya mataifa ya eneo ni mwenge usioweza kuzimwa

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema muqawama na mapambano ya mataifa yaliyoamka ya eneo ni mwenge usioweza kuzimwa na kusisitiza kuwa: " Jibu la Wayemen ambalo ni onyo linapaswa kuwa somo kwa maadui wa eneo ili wasitishe vita katika eneo."

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  ameyasema hayo leo Jumatano mjini Tehran katika kikao cha baraza la mawaziri na kuongeza kuwa: "Wasiolitakia mema eneo wanaanza kutoa tuhuma badala ya kukiri kuhusu uwezo mkubwa wa Hizbullah ya Lebanon, Al Hashd al Shabi ya Iraq na wananchi wa Syria na Yemen."

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria kuhusu kuuawa watu wasio na hatia huko Yemen na kudondoshewa mabomu mahospitali, nyumba na shule za nchi hiyo na kuongeza kuwa: "Watu adhimu, waangalifu na walio macho wa Yemen hawakuanzisha mapigano bali ni Saudia, Imarati, Wamarekani, baadhi ya nchi za Ulaya na utawala wa Kizayuni ndio walioanzisha vita katika eneo na kuiharibu Yemen."

Rais Rouhani amesisitiza kuwa, Iran haitaki mapigano yaibuke katika eneo na kuongeza kuwa: "Kama ambvyo Iran ina uhusiano mzuri, wa kidugu na kirafiki na majirani zake katika maeneo ya kaskazini, mashariki na magharibi pia inataka uhusiano mzuri na majirani zake katika maeneo ya kusini."

Rais Rouhani katika kikao cha baraza la mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha ameashiria uhusiano wa kibenki baina ya Iran na nchi kadhaa pasina kutegemea mfumo wa kimataifa wa kifedha wa SWIFT unaosimamiwa na Marekani na kusema: "Uhusiano wa kibiashara na kiuchumi na Iran kwa kutegeme sarafu za kitaifa za Uturuki, Russia na Iraq ni nukta ambayo inaweza kuondoa matatizo mengi katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara. Rais wa Iran amesema hivi sasa katika uga wa kimataifa kuna mkakati wa kuondoa mabadilishano ya kifedha kwa kutegemea dola ya Marekani. Amesema kwa kuendelea mchakato huo, ubabe wa Marekani katika masoko ya kifedha ya kimataifa utazidi kudhoofika.

Tags

Maoni