Oct 20, 2019 11:40 UTC
  • Zanganeh: Juhudi za kusitisha ustawi wa sekta ya mafuta ya Iran zimefeli

Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa ustawi wa sekta ya mafuta ya Iran si tu kuwa haujasitishwa bali kusainiwa makubaliano na kutekelezwa miradii mingi katika sekta ya mafuta na gesi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kumeongezeka.

Bijan Namdar Zanganeh ameongeza kuwa, ingawa juhudi kubwa zimefanywa ili kusitisha ustawi wa sekta ya mafuta ya nchi hii katika kipindi hiki cha vikwazo; lakini ustawi wa sekta hiyo umeongezeka. Ameendelea kubainisha kuwa, uchimbaji mafuta na gesi ya Iran unaendelea; na wakati wowote kunapogunduliwa uchimbaji mpya wananchi hupewa taarifa ikiwa ni habari njema kwao inayoashiria kuongezeka akiba ya mafuta na gesi inayoweza kutumika. 

Sekta ya mafuta ya Iran inazidi kukua licha ya vikwazo

Kuhusu madai ya Saudi Arabia kwamba imerejea kikamilifu uzalishaji wake wa mafuta katika muda wa chini ya mwezi mmoja; Waziri wa Mafuta wa Iran amesema kuwa: Suala hilo linaonyesha kuwa taarifa zilizotolewa awali kwamba, Saudia ilisimamisha uzalishaji wake wa mapipa milioni tano au sita ya mafuta kwa siku, hayakuwa na ukweli wowote, bali ilikuwa ni propaganda za kisiasa tu, kwa sababu ni muhali kwa vituo ambavyo vilikuwa vikizalisha kiwango hicho cha mafuta kwa siku, kuweza kufanyiwa ukarabati wa wiki mbili au tatu tu, baada ya kushambuliwa na kuharibiwa vibaya.  

 

Tags

Maoni