Oct 21, 2019 12:29 UTC
  • Dakta Zarif: Niko tayari kuelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutatua hitilafu zilizopo

Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inapokea kwa mikono miwili ubunifu wowote ule wenye lengo la kuhitimisha vita nchini Yemen na kwamba, yupo tayari kufanya safari nchini Saudi Arabia endapo mazingira yataandaliwa.

Dakta Muhammad Javad Zarif ametangaza kuwa, Iran daima ipo pamoja na taifa la Yemen na inaamini kwamba, kusimamishwa vita katika hatua ya awali kutakuwa na msaada kwa taifa hilo lililoharibiwa vibaya na vita.

Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa na Kanali ya Televisheni ya al-Masira, Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kunaendelea mawasiliano na mashauriano na Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan kuhusiana na hali ya mambo nchini Yemen.

Dakta Zarif amesisitiza kuwa, Iran inakaribisha kwa mikono mwili mpango na ubunifu wowote ule wenye lengo la kupunguza mivutano katika eneo na kwamba, itatoa kikamilifu ushirikiano wake kwa hatua na mpango wowote ule wenye lengo la kuhitimisha vita nchini Yemen.

Mashambulio ya anga ya Saudi Arabia na washirika wake yanavyoiboa vibaya Yemen

Mashambulioi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia ikisaidiwa na Marekani na washirika wao dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Yemen tokea Machi mwaka 2015 yameua maelfu ya raia na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. 

Aidha hujuma hiyo ya kijeshi imeharibu sehemu kubwa ya miundombinu na kuifanya nchi hiyo ikabiliwe na maafa makubwa ya kibinadamu.

Maoni