Dec 07, 2019 04:04 UTC
  • Muhammad Javad Zarif
    Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekemea majaribio ya kombora linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia yaliyofanywa na utawala haramu wa Israel na amezikosoa vikali Marekani na nchi za Ulaya kutokana na kunyamaza kimya mbele ya maghala ya silaha za nyuklia za utawala huo.

Muhammad Javad Zarif amesema kwamba, Israel imefanya majaribio ya kombora lenye uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia ambalo lengo lake ni Iran. Ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Nchi tatu za Ulaya yaani Uingereza, Ujerumani na Ufaransa pamoja na Marekani kamwe hazilalamiki kuhusiana na maghala pekee la silaha za nyuklia katika eneo la magharibi mwa Asia ambayo yana uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia lakini daima zinaghadhibika kuhusiana na silaha za kujihami za Iran.

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel jana Ijumaa viliripoti kwa, vyombo vya usalama vya utawala huo vimefanyia majaribio kombola la masafa ya mbali aina ya Jericho 4 linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia. Utawala wa Kizayuni ambao umefanya majaribio ya kombora hilo linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia daima imekuwa ukilalama kuhusiana na majaribio ya makombora ya kujihami ya Iran na kutoa wito wa kuwekwa vikwazo dhidi ya Tehran. 

Kombora la Jericho 2 la Israel

Duru za kuaminika zinaamini kwamba, utawala ghasibu wa Israel unamiliki vichwa 80 hadi 400 vya makombora ya nyuklia. Utawala huo pia umekataa kuwaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuingia katika taasisi zake za nyuklia na umegoma kutia saini hati ya makubaliano ya kuzuia silaha za nyuklia NPT.   

Tags

Maoni