Dec 07, 2019 12:16 UTC
  • Iran yazindua drone mpya  yenye uwezo mkubwa wa kivita

Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua ndege mpya isiyo na rubani (drone) yenye uwezo mkubwa wa kioparesheni na kivita.

Drone hiyo mpya imezinduliwa leo katika mji wa Konarak mkoani Sistan na Baluchestan katika eneo la kusini mashariki mwa Iran.

Sherehe za uzinduzi wa drone hiyo iliyopewa jina la 'Simorgh' imehudhuriwa na Admeli Habibullah Sayyari, Mratibu Mkuu wa Jeshi la Majini la Iran na Admeli Hussein Khanzadi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Majini la Iran.

Admeli Hussein Khanzadi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Majini la Iran

Drone ya Simorgh ina uwezo wa kuruka umbali wa kilomita 1500 na kutekeleza oparesheni za kijeshi zikiwemo za mapigano na vita vya kielektroniki.

Aidha drone ya Simorgh inaweza kuruka kwa masaa 24 katika urefu wa mita 25,000.

Maoni