Dec 09, 2019 12:24 UTC
  • Mousavi: Iran itatoa jibu la kujutisha kwa uchokozi wa aina yoyote ile

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Iran itatoa jibu kali na la kujutisha kwa uchokozi wa aina yoyote au hatua yoyote ile ya kipumbavu itakayochukuliwa dhidi yake.

Sayyid Abbas Mousavi ametoa kauli hiyo leo kujibu madai na vitisho vya kufanya hujuma na mashambulio ya kijeshi vilivyotolewa na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni, akiwemo waziri wa mambo ya nje na waziri wa vita wa utawala huo, katika siku chache zilizopita wamekuwa wakiropokwa na kupayuka kauli za kutishia kuishambulia kijeshi Iran.

Akijibu matamshi hayo ya vitisho ya Wazayuni, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: Kwa kutegemea nguvu na uwezo wake uliojengeka juu ya utamaduni wa watu wake, wa muqawama na kujitolea mhanga, Iran haitachelea wala kusita hata chembe kuchukua hatua za kulinda ardhi na usalama wa taifa lake.

Mousavi ameeleza kwamba, vitisho vilivyotolewa na utawala unaoikalia Quds tukufu kwa mabavu ni ishara ya udhaifu na kutokuwa na uwezo; na vitisho hivyo vimetolewa ili kufifisha migogoro na matatizo ya ndani yanayowakabili viongozi wa utawala huo. Aidha ameongeza kuwa: Dhati na utambulisho wa utawala wa Kizayuni katika muda wote wa miaka 70 ya uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu vimejengeka juu ya msingi wa vitisho na uchokozi.../  

Tags

Maoni