Dec 13, 2019 12:51 UTC
  • Sayyid Abbas Mousavi
    Sayyid Abbas Mousavi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imejibu matamshi yaliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani akisema kuwa matamshi kama hayo yanayoingilia masuala ya ndani ya Iran hayaweza kuficha makosa ya baadhi ya nchi za Ulaya ya kutotekeleza majukumu yao katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na misimamo yao isiyo sawa kuhusiana na ugaidi wa kiuchumi wa Marekani.

Sayyid Abbas Mousavi amesema ilitarajiwa kwamba, ilitarajiwa kwamba Berlin ingeheshimu misingi ya awali ya haki za binadamu badala ya kuwa na sera za upendeleo dhidi ya Iran.

Amesema Jamhuri ya Kiislamu inaipa umuhimu mitazamo na ukosoaji wa raia wake na kwamba katika machafuko ya hivi karibuni hapa nchini Iran inatenganisha baina mitazamo ya wananchi waliokuwa wakiandamana na maadu, watu walihusika na mauaji ya wananchi na wafadhili wao wa kigeni. Amesema Tehran itachukua maamuzi ya dharura katika kuheshimu haki za wananchi na kudhamini usalama wao kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi uliofanyika hapa nchini kuhusiana na kadhia hiyo.

Vilevile amemwambia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Mass kwamba, dunia haijasahau nchi iliyompa dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein silaha za kemikali zilizotumiwa kuua raia wa Irani na wenzao wa Iraq wakati wa vita vya kulazimishwa vya Saddam Hussein dhidi ya Iran.

Silaha za kemikali za Ujerumani zilitumiwa na Saddam Hussein kuua raia wasio na hatia

Vilevile amemtaka Mass akumbuke jinsi polisi ya Ujerumani ilivyowakandamiza waandamanaji mkesha wa mkutano wa G20 katika mji wa Hamburg Julai mwaka 2017.

Akuhutubia Bunge jana Alkhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Mass alidai kuwa, mamia ya watu waliuawa katika machafuko ya hivi kibuni nchini Iran na kwamba kuna ulazima wa kulaaniwa ukandamizaji uliofanyika dhidi ya maandamano ya wananchi.

     

Tags

Maoni