Jan 16, 2020 02:31 UTC
  • IRGC: Iran imefanikiwa kudhibiti uwezo na nguvu za Marekani

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria wimbi la hivi karibuni la ushindi wa Iran dhidi ya Marekani na kusema kuwa, "Jamhuri ya Kiislamu imefanikiwa kuidhalilisha na kuzidhibiti nguvu za Marekani."

Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda wa IRGC alisema hayo jana Jumatano katika mkoa wa Bushehr kusini mwa nchi na kufafanua kuwa,"Katika miaka 41 ya historia ya taifa la Iran ya Kiislamu katika mapambano dhidi ya maadui, tumeshuhudia kurasa zinazong'aa za ushindi wa kipekee na wa kistratajia wa taifa hili."

Amesema taifa la Iran limefanikiwa kuvunja sera haribifu za adui katika eneo (Asia Magharibi) na kote duniani, na hii leo dunia nzima inashuhudia matunda ya kusimama kidete huko bila kutetereka Jamhuri ya Kiislamu.

Makombora ya Iran; Sehemu ya uwezo wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani ilimuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Quds cha SEPAH ili kufidia wimbi la kufeli na kushindwa kwake, lakini hata hivyo mambo yaligeuka na kuwa kinyume na matarajio yao.

Meja Jenerali Hossein Salami ameongeza kuwa, "Taifa kubwa la Iran limefanikiwa kumdhalilisha adui Marekani na hii leo tunashuhudia namna nguvu za taifa hilo zinavyopuputika na kuporomoka."

Tags

Maoni