Jan 17, 2020 07:57 UTC
  • Maelfu ya Wairani washiriki Sala ya Ijumaa chini ya uimamu wa Kiongozi Muadhamu

Maelfu ya wananchi Waislamu wa Iran wamekusanyika katika eneo la Musalla wa Imam Khomeini (MA) hapa jijini Tehran wakisubiri hotuba na Sala ya Ijumaa zitakazoongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei anatazamiwa kuongoza Sala ya Ijumaa ya leo hapa mjini Tehran, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo baada ya kupita miaka minane.

Tangu nyakati za asubuhi, maelfu ya wananchi wa Iran kutoka pembe mbalimbali za Tehran walianza kuelekea katika ukumbi huo wa Sala wa Musalla wa Imam Khomeini (MA) ambao hivi sasa umefurika hadi pomoni.

Baadhi ya wananchi wa Iran wameleekea kwenye ukumbi huo kwa makundi, huku wengine wakiwa wamebeba mabango yenye picha za Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC aliyeuawa hivi karibuni katika shambulizi la kigaidi la Marekani nchini Iraq.

Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Wachambuzi wa kisiasa wanasema matukio ya hivi sasa ya kieneo na kuuawa shahidi Jenerali Soleimani ni katika maudhui zitakazogusiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa ya leo hapa Tehran.

Mara ya mwisho Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kuongoza Sala ya Ijumaa hapa nchini ilikuwa mwaka 2012.

Tags

Maoni