Jan 17, 2020 15:49 UTC
  • Russia: Wakati ndege ya Ukraine ilipoanguka, ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani karibu na Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wakati tukio la kuanguka kwa ndege ya abiria ya Ukraine mjini Tehran likijiri, kwa akali ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani zikiruka karibu na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sergey Lavrov ameyasema hayo leo katika kikao chake cha kila mwaka na waandishi wa habari ambapo ameongeza kwa kusema: "Tunazo taarifa zinazoonyesha kwamba kwa akali ndege sita za kivita za F 35 za Marekani zilikuwa zikipaa karibu na mikaka ya Iran." Itakumbukwa kuwa ndege moja ya abiria mali ya Shirika la Ndege la Ukraine ilianguka siku ya Jumatano ya tarehe 8 Januari karibu na Uwanja wa Ndege wa Imam Khomeini (MA) mjini Tehran, na kupelekea kufariki dunia watu wote waliokuwa ndani yake. Kufuatia tukio hilo chungu jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lilitoa taarifa ambayo sambamba na kuashiria kwamba kulikuwepo na ndege za kivita za jeshi la kigaidi za Marekani karibu na mipaka ya Iran, ilisema kuwa kosa la kibinaadamu pamoja na ndege hiyo kubadili mwelekeo wake na pia kukaribia kwake kwenye eneo nyeti la kijeshi la nchi hii, ni sababu iliyopelekea kutunguliwa kwake.

Sergey Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia 

Katika kiko hicho na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia sambamba na kutoa onyo kali kuhusiana na njama za nchi za Ulaya za kujaribu kuitwisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lawama inayohusu mustakbali wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA amesema kuwa, nchi tatu za Ulaya zilizoshiriki mapatano hayo zimeamua kusalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani kwa kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kusisitiza kuwa hiyo inabainisha kwamba madola hayo yanakusudia kuitwisha Tehran dhima ya kufeli huko. Ameongeza kwa kusema, wakati Iran inaposema kuwa imesimamisha utekelezaji wa majukumu yake ya kujitolea katika JCPOA, Moscow inafahamu vyema uamuzi huo wa Iran. Maelezo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia kuhusiana na kadhia ya tukio la kuanguka ndege hiyo mali ya Ukraine, inabainisha kuwepo kwa njama za makusudi za Marekani za kuiangusha ndege hiyo.

Maoni