Feb 16, 2020 16:25 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman: Iran ni nchi kubwa katika eneo la magharibi mwa Asia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesisitiza kuwa, Iran ni nchi kubwa katika eneo la magharibii mwa Asia.

Yusuf bin Alawi Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema katika Mkutano wa Usalama wa Munich kwamba kutoa changamoto kwa Iran hakusaidii kutuliza hali ya mambo katika eneo hili kwa sababu Iran itaendelea kuwa nchi kubwa katika kila hali. Bin Alawi ameeleza jinsi Oman na Iran zinavyoishi pamoja kwa amani na kusisitiza misimamo ya Mfalme wa Oman ya kuunga mkono amani na utulivu katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Ufunguzi wa Mkutano wa Usalama wa Munich 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman amesema kuwa, nchi yake ina wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutokea makosa yoyote baina ya meli za kivita katika Lango la Hormoz na hivyo kusababisha matatizo makubwa. Matamshi hayo ya Bin Alawi yameashiria muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi uliopewa jina la "Oparesheni za Sentinel" unaoundwa na nchi saba katika maji ya Ghuba ya Uajemi.

Marekani imezidisha uwepo wa wanajeshi wake katika eneo la Ghuba ya Uajemi katika miezi ya karibuni lengo likiwa kuzidisha mashinikizo dhidi ya Iran. na inashirikiana na washirika wake kufanya uchochezi dhidi ya jamhuri ya Kiislamu. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepinga tuhuma za Washington na London kwamba imekiuka uhuru wa safari za meli katika Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, Iran na majirani zake ndizo zenye jukumu kuu la kulilinda eneo hilo na hazitotoa mwanya wa kuyumbishwa hali ya usalama katika Ghuba ya Uajemi. 

Tags

Maoni