Feb 21, 2020 15:03 UTC
  • Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Kaulimbiu ya

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran, amesema, wananchi wa Iran wameifanya ithibiti sha'ar na kaulimbiu ya "Mauti kwa Marekani" kwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa Majlisi ya 11 ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) na uchaguzi mdogo wa Baraza la 5 la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.

Ayatullah Ahmad Khatami amesema, kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi wa leo kumemuudhi na kumkasirisha adui na akaongezea kwa kusema: Maadui na vyombo vya habari vyenye mfungamano nao walikuwa wakiwasihi na kuwabembeleza wananchi wa Iran wasishiriki katika uchaguzi, lakini kwa kushiriki, tena kwa wingi, wananchi wa Iran wametoa jibu kali kwa maadui na vyombo vyao vya habari.

Ayatullah Ahmad Khatami amesisitiza kuwa: Kushiriki wananchi katika uchaguzi kumewadhalilisha maadui na kuwapa heshima wananchi wa Iran.

Baadhi ya wananchi wakishiriki katika zoezi la upigaji kura

Katika sehemu nyingine ya hotuba zake, Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amegusia pia matukio ya eneo la Asia Magharibi na akasema: Adui alikuwa anadhani, kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kambi ya mapambano na Muqawama itadhoofika, lakini kugonga mwamba njama za Marekani katika nchi za Iraq na Lebanon na kurudi nyuma magaidi wa kitakfiri kutoka viunga vya mji wa Aleppo (Halab) Syria na kuweza kutua ndege ya abiria katika mji huo baada ya miaka tisa ni miongoni mwa habari za kufurahisha za Muqawama katika siku za karibuni.

Aidha Ayatullah Khatami amesema, Muamala wa Karne ni mpango uliofeli kikamilifu na akasisitiza kuwa, Marekani na Wazayuni hawatoupata utulivu katika eneo.../ 

Maoni