Feb 22, 2020 02:44 UTC
  • Wairani wakipiga kura
    Wairani wakipiga kura

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa radimali yake kufuatia hatua ya Marekani ya kuwawekea vikwazo wanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa, serikali, taifa na nguzo zote za Jamhuri ya Kiislamu haziipi thamani Marekani wala vikwazo vyake vya kidhalimu.

Sayyid Abbas Mousavi amesema kitendo hicho cha kuwawekea vikwazo maafisa wa uchaguzi kinadhihirisha namna sera ya Marekani ya mashinikizo ya kiwango cha juu ilivyogonga mwamba mkalaba wa taifa kubwa la Iran, na inaonyesha pia namna Marekani inavyoogopa demokrasia na ushiriki wa wananchi wa Iran kwenye michakato ya kidemokrasia hapa nchini.

Ameeleza bayana kuwa, "Hao waliowawekea vikwazo, ugaidi wa kiuchumi na mashinikizo ya hali ya juu Wairani milioni 83 wameshindwa kupata mafanikio waliotarajia kwa vitendo vyao hivyo. Jibu la Iran kwa mashinikizo ya kiwango cha juu ni muqawama na mapamabano ya hali juu, na bila shaka Wamarekani watasalimu amri mkabala wa taifa la Iran."

Wakati huohuo, Katibu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameijekeli hatua hiyo ya Washington ya kuwawekea vikwazo maafisa wa Baraza hilo kwa madai yasiyokuwa na msingi, ambapo amesema kwa dhihaki, "Sasa hatuwezi kwenda Marekani tena kusherehekea Krismasi na kutoa na kutumia pesa zetu (kutokana na vikwazo hivyo."

Kauli hiyo ya Ayatullah Ahmad Jannati muda mfupi baada ya kupiga kura jana Ijumaa ya kuikejeli serikali ya Washington iliwavunja mbavu waandishi wa habari wa ndani na nje ya Iran, wanaofuatilia zoezi hilo la kidemokrasia. 

Ayatullah Jannati, Katibu wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akipiga kura

Wizara ya Fedha ya Marekani inadai imewawekea vikwazo wanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na Kamati ya Kusimamia Uchaguzi nchini eti kwa kuwaondoa kwenye kinyang'anyiro baadhi ya wagombea. Vyombo hivyo vya uchaguzi Iran viliwaondoa baadhi ya wagombea hao kwa kushindwa kutimiza vigezo na masharti yaliyoanishwa na katiba na sheria za nchi.

Mamilioni ya wananchi wa Iran walishiriki katika Uchaguzi wa Bunge la 11 la Iran linalojulikana kwa jina la Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu na uchaguzi wa kwanza mdogo wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu uliofanyika jana Ijumaa kote nchini.

Tags

Maoni