Feb 26, 2020 07:24 UTC
  • Shamkhani:  Kirusi cha Corona kinatumika kuzidisha mashinikizo dhidi ya Iran

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameashiria njama mpya dhidi ya Iran kwa kisingizio cha kirusi cha Corona na kusema: "Imepengwa kuwa stratijia ya mashinikizo ya juu kabisa dhidi ya Iran ikamilishwe kwa kirusi cha Corona."

Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran Jumanne usiku aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Mashinikizo ya kisaikolojia kwa nchi za eneo ili zifunge mipaka yao ya nchi kavu na angani na kueneza hadaa kuwa eti Iran inaficha ukweli ni mbinu mpya inayotumiwa na adui."

Shamkhani pia amejibu matamshi ya uingiliaji ya Mike Pompeo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuhusu idadi ya walioambukizwa Corona nchini Iran na kusema: "Pompeo anatoa madai kuwa eti Iran inaficha habari kuhusu Corona katika hali ambayo Marekani haijatoa taarifa sahihi kuhusu ukweli wa yaliyojiri huko Ainu Assad, kuanguka ndege yake ya kijasusi nchini Afghanistan na idadi kubwa ya Wamarekani waliopoteza maisha kutokana na homa ya  mafua mwaka huu." 

Maafisa wa afya walio mstari wa mbele kukabiliana na Corona

Homa ya kirusi cha Corona iliripotiwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan mkoani Hubei mashariki mwa China na sasa mbali na kuathiri mikoa 30 ya nchi hiyo homa hiyo imeenea katika zaidi ya nchi 30 zikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Australia, Italia, Thailand, Korea Kusini, Japan, Canada, Ufaransa, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudi Arabia,

Kwa mujibu wa Takwimu hadi sasa watu zaidi ya 80, elfu wameabukizwa Corona kote duniani, wengi wakiwa nchini China ambapo zaidi ya 30000 wamepona na wengine 2700 wamepoteza maisha.

Maoni