Feb 27, 2020 13:04 UTC
  • Kiongozi Muadhamu apongeza jitihada za wahudumu wa afya nchini za kupambana na Corona

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza jitihada zinazofanywa na maafisa na wahudumu wa afya hapa nchini kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona.

Katika mkutano wake na Rais wa Akademia ya Sayansi za Matibabu ya Iran mapama leo, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amewapongeza Waziri wa Afya, madaktari, wauguzi na wahudumu wengine wa sekta ya afya hapa nchini kwa kufanya juu chini kuhakikisha kuwa wanadhibiti maambukizi ya virusi hivyo sambamba na kutoa huduma za tiba kwa waathiriwa.

Katika mkutano huo na Rais wa Akademia ya Sayansi za Matibabu ya Iran, Seyyed Alireza Marandi, Kiongozi Muadhamu amewahutubu wahudumu wa afya wa Iran kwa kusema, "kazi yenu ina thamani kubwa. Jitihada zenu zimenyanyua thamani ya kazi ya matabibu na wauguzi."

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameongeza kuwa, kitu cha muhimu zaidi kuhusu taaluma ya utabibu ni malipo makubwa yanayowasubiri wahudumu wa afya kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Kiongozi Muadhamu na Sayyed Alireza Marandi

Wakati huohuo, Wizara ya Afya ya Iran imesema idadi ya watu walioaga dunia hapa nchini kutokana na virusi vya Corona imefikia watu 26, huku idadi ya waathirika ikifika 245.

Madaktari, wauguzi na wahudumu wengine wa sekta ya afya katika mikoa 20 ya Iran wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kutibu na kudhibiti Corona hapa nchini. 

  

Tags

Maoni