Mar 22, 2020 07:32 UTC
  • Iran yakanusha madai ya uongo ya Marekani kuhusu vikwazo vya dawa na chakula

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha vikali madai ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyodai kuwa eti vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran havihusu dawa na chakula.

Katika ujumbe wake wa hivi karibu kwa njia ya Twitter, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imedai kwamba chakula, madawa na misaada ya kibinadamu haimo katika orodha ya vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran. Ujumbe wa Twitter wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani ulisema: "Wairani wapendwa, huu ni ukumbusho wa kirafiki: Chakula, dawa na misaada ya kibinadamu haijawekewa vikwazo."

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na taifa la Iran limetia nia ya kweli ya kuvisambaratisha vikwazo vya Marekani

 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran jana Jumamosi ilijibu madai hayo ya uongo ya Marekani na kuandika katika ukurasa wake wa Twitter maneno yasemayo: "Wairani na Wamarekani wapendwa, huu ni ukumbusho wa kiurafiki, kama yeyote kati yenu atafanikiwa kutuma kitu chochote nchini Iran kutoka nyumbani kwake, au kupitia shirika au benki ya karibu na anapoishi iwe ni paketi ya dawa za Advil au kilo ya adesi au mask japo moja - kama ataweza kutuma chochote kwa ajili ya jamaa zake nchini Iran - basi nyaraka na risiti yake aitume kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani."

Hivi karibuni pia, Dk Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutilia mkazo wajibu wa kuondolewa na kufutwa vikwazo vyote vya upande mmoja vya Marekani vilivyo kinyume cha sheria dhidi ya Iran akisema kuwa, licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kupiga hatua kubwa za kielimu, lakini vikwazo vya Marekani vinaifanya Iran ikumbwe na kikwazo kikubwa katika kupambana na kirusi cha corona.

Tags

Maoni