Mar 23, 2020 09:15 UTC
  • Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; viongozi wa Marekani ndio watuhumiwa wa kuzalisha corona

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia ugonjwa wa COVID-19 ulioenea dunia nzima na kukataa msaada wowote wa Marekani kwa Iran akisema kuwa, viongozi wa Marekani ndio watuhumiwa wa kuzalisha kirusi cha corona hivyo si watu wa kuaminika na kwamba mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kukubali msaada wao.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei siku ya Jumapili ya tarehe 22 Machi 2020 alilihutubia taifa la Iran kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa sikukuu ya Mab'ath ya kupewa Utume Mtume Muhammad SAW na sikukuu ya Nairuzi. Amma kuhusu madai ya viongozi wa Marekani ya eti wako tayari kuisaidia dawa na vifaa vya tiba Iran amesisitiza kuwa: Kwanza wenyewe Wamarekani wana upungufu mkubwa wa dawa na vifaa vya kujikingi na corona, pili ni kwamba wakati Wamarekani ndio watuhumiwa wa kuzalisha kirusi cha corona, mtu gani mwenye akili zake timamu atakubali kupokea msaada wao?

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, viongozi wa Marekani ni waongo na ni magaidi. Aidha amesema: Hatuna imani hata kidogo na Wamarekani kwani wanaweza kutuma dawa zitakazopelekea kuongezeka maambukizi ya corona nchini Iran na kuyafanya yabakie milele. 

Vita dhidi ya corona nchini Iralia. Nchi hiyo ya Ulaya ndiyo iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa COVID-19 hivi sasa

 

Baada ya maambukizi ya kirusi cha corona kuenea nchini China na kufika pia nchini Iran, taarifa kuhusu kuhusika Marekani katika kuzalisha kirusi cha corona zilipata nguvu hasa baada ya viongozi wa China kuituhumu Marekani kuwa ndiyo iliyoingiza ugonjwa huo nchini mwao. 

Kabla ya hapo Robert Redfield, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani alikuwa amesema kuwa, kirusi cha corona kiligunduliwa na maafisa wa afya wa Marekani (kabla ya China), hivyo chanzo kikuu cha kirusi hicho si China.

Baada ya kutolewa msimamo huo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China alisema, kuna uwezekano jeshi la Marekani ndilo lililopeleka kirusi cha corona katika mji wa Wuhan huko China. Baada ya kutolewa madai hayo, Taasisi ya Ulinzi Usio wa Kutumia Silaha ya Iran hivi karibuni iliitisha kikao maalumu cha kujadili uwezekano kuwa kirusi cha corona kimezalishwa na kuenezwa kwa makusudi.

Alaakullihaal, madai ya viongozi wa Marekani kuhusiana na Iran baada ya kuenea kirusi cha corona ni ya kinafiki na sababu yake ni kwamba kwa upande mmoja, viongozi wa Marekani wanadai wako tayari kuwasaidia wananchi wa Iran lakini wakati huo huo wanaendelea na vikwazo vyao vya kiwango cha juu kabisa dhidi ya taifa hili bila ya kujali haki ya wananchi wa Iran ya kuishi na kuwa salama, haki ambayo ni ya kimsingi kabisa kwa kila mwanadamu.

Rais wa Marekani, Donald Trump ndiye mtuhumiwa wa kueneza kirusi cha corona duniani

 

Vikwazo vya kiwango cha juu kabisa vya Marekani vinakwenda sambamba na kuenea kirusi hatari cha corona humu nchini kiasi kwamba kila baada ya dakika 10 raia mmoja wa Iran anapoteza maisha kwa kirusi hicho ambacho Marekani ndiye mtuhumiwa wa kukizalisha na kukieneza. Hivyo vitendo vya viongozi wa Marekani ni jinai dhidi ya ubinadamu au kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, viongozi wa Marekani ni magaidi wenye roho ngumu.

Ukweli ni kuwa corona ni janga la dunia nzima kutokana na kwamba hivi sasa kirusi hicho hatari kimeshaenea katika zaidi ya nchi 180 duniani, hivyo kunahitajika ushirikiano wa watu wote kukabiliana na ugonjwa huo wa COVID-19.

Licha ya kuwa Iran imepiga hatua kubwa za kielimu, kisayansi na kiteknolojia, na licha ya kwamba ina vifaa vya kisasa kabisa vya tiba na imeweza kuonesha uwezo wake mkubwa wa kupambana na kirusi cha corona, lakini kama ambavyo amekuwa akisisitiza mara kwa mara Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, kwamba vikwazo vya kidhulma na vya kigaidi vya Marekani dhidi ya Iran ni kikwazo katika vita dhidi ya COVID-19 humu nchini. Pamoja na hayo, protocoli za tiba nchini Iran kama vile mpango wa taifa wa kujitolea watu wote humu nchini kupambana na kirusi cha corona zimeungwa mkono na kupongezwa na hata na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Utafiti wa kitiba uliokaribia mno kuzaa matunda ya kuzalishwa dawa mpya ya kutibu ugonjwa wa corona ni hatua nyingine ya kijihadi ya madaktari bingwa wa Iran.

Ni jambo lililo wazi kwamba kwa kuchungwa kikailifu protokali za tiba na kuchukuliwa hatua zinazofaa na wananchi, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, changamoto ya corona itaondoka na jambo hilo litathibitisha kwa mara nyingine kwamba nguvu na uimara wa Iran hauko katika upande wa kiulinzi na kijeshi tu, lakini ni mkubwa pia katika upande wa tiba, elimu na uchumi.

Tags