Mar 25, 2020 13:18 UTC
  • Dakta Zarif: Umoja wa Ulaya unaiunga mkono Iran katika kukabiliana na virusi vya Corona

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Umoja wa Ulaya unaliunga mkono taifa hili katika kupambana na virusi vya Corona.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Gordan Grlić-Radman, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Croatia ambaye nchi yake ni mwenyekiti wa kiduru wa Umoja wa Ulaya na kueleza kwamba, umoja huo unaiunga mkono pia Iran katika suala la kuondolewa vizingiti vya kifedha kwa minajili ya kurahisisha vita dhidi ya virusi vya Corona.

Katika mazungumzo yake na Dakta Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Croatia sambamba na kutoa ripoti kuhusu kikao cha Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya kilichofanyika hivi karibuni amesema kuwa, umoja huo unaiunga mkono Iran katika kupambana na virusi vya Corona.

Vikwazo vya upande mmoja na vya kidhalimu vya Marekani vimekuwa kikwazo kikubwa kwa sasa hapa nchini Iran katika juhuudi za taifa hili la kukkabiliana na virusi vya Corona.

Vikwazo hivyo ambavyo vimekuwa vikijumuisha pia bidhaa muhimu kama dawa na suhula za kitiba vimeendelea kulalamikkiwa na mataifa mbalimbali ya dunia yakieleza kwamba, hatua hiyo ya serikali ya Marekani inakinzana waziwazi na utu na ubinadamu hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na virusi hatari vya Corona.

Tags

Maoni