Mar 26, 2020 08:13 UTC
  • Barua ya nchi 8 kwa Katibu Mkuu wa UN: Vikwazo vina taathira hasi kwa udhibiti wa janga la corona

Wawakilishi wa Iran, Russia, China, Cuba, Korea Kaskazini, Iraq, Venezuela na Nicaragua katika Umoja wa Mataifa wamemwandikia barua Katibu Mkuu wa umoja huo, ambapo mbali na kuashiria kuwa corona ni adui wa pamoja wa nchi zote, wametahadharisha kwamba, vikwazo vina taathira hasi kwa udhibiti wa maambukizi ya kirusi hicho.

Katika barua yao hiyo kwa Antonio Guterres, wawakilishi wa nchi hizo nane wamebainisha kuwa, hatua za utumiaji nguvu na za upande mmoja, zisizo za kisheria na zenye kukiuka waziwazi sheria za kimataifa na Hati ya Umoja wa Mataifa ambazo zinachukuliwa dhidi ya nchi kadhaa hivi sasa, zinatatiza na kukwamisha juhudi za nchi hizo za kukabiliana na janga la corona.

Ikiashiria ripoti ya wataalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa inayoeleza kwamba, utumizi wa hatua za nguvu za upande mmoja unaiathiri theluthi nzima ya jamii ya wanadamu barua hiyo imesisitiza kwamba: Haifai kuruhusu malengo na matashi ya kisiasa yakwamishe juhudi za kuokoa maisha ya watu.

Iran ni nchi inayokabiliwa na vikwazo haramu na vya kidhalimu vya Marekani

Sehemu nyingine ya barua hiyo ya wawakilishi wa nchi nane wanachama wa Umoja wa Mataifa imekumbusha kuwa, kukabiliana na janga la corona kunahitaji mshikamano, ushirikiano na nchi kusaidiana kwa kiwango cha juu kabisa na ikasisitiza kwamba, uwekaji vikwazo unadhoofisha jitihada mtawalia zinazofanywa na serikali za mataifa kwa ajili ya kupambana na corona hususan katika uandaaji athirifu na kwa wakati wa zana na vifaa vya utabibu vikiwemo vifaa vya kupimia na dawa zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa.

Wawakilishi wa Iran, Russia, China, Cuba, Korea Kaskazini, Iraq, Venezuela na Nicaragua katika Umoja wa Mataifa wamemtaka Katibu Mkuu wa umoja huo ahakikishe, vikwazo hivyo haramu, vya uchukuaji hatua bila kujali na vyenye kutoa mbinyo na mashinikizo ya kiuchumi, vinaondolewa kikamilifu na kwa haraka.../

 

Tags

Maoni