Apr 07, 2020 23:41 UTC
  • Zarif: Iran haihitaji sadaka ya Trump; Marekani iache kuzuia uuzaji wa mafuta ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina haja na sadaka ya serikali ya Marekani na kusisitiza udharura wa kuondolewa vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran.

Muhammad Javad Zarif ameeleza katika ukurasa wake wa Twitter namna Iran ilivyo na utajiri wa rasilimali watu na maliasili na kusema kuwa Jamhuri ya Kiislamu haina haja ya sadaka ya Donald Trump ambaye amelazimika kununua vifaa vya kusaidia kupumia kutoka nchi alizoziwekea vikwazo. 

Rais Donald Trump wa Marekani  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekumbusha kuwa Tehran inamtaka Rais wa Marekani asizuia uuzaji wa mafuta na bidhaa nyingine za Iran  na pia asiizuie nchi hii kununua mahitaji yake na kujiingizia kipato.  

Marekani ingali inaendeleza misimamo yake ya vikwazo katika fremu ya siasa za mashinikizo na vikwazo vya hali ya juu dhidi ya Iran licha ya dunia kukumbwa na maambukizi ya virusi hatari vya corona na ulazima wa  pande zote kushirikiana katika mapambano dhidi ya janga hili. 

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa hadi sasa watu 3,872 kati ya jumla ya watu 62,589 walioambukizwa virusi vya corona nchini Iran, wameaga dunia.   

Maoni