May 21, 2020 05:59 UTC
  • Iran: Mpango wa

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, mpango wa Marekani-Israel wa 'Muamala wa Karne" ni ishara ya wazi ya hila na utapeli wa Wamarekani.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri nyay Kigeni ya Jamhuri ya KIiislamu ya Iran iliyotolewa kwa mnasaba wa kukaribia Siku ya Kimataifa ya Quds itakayoadhimishwa kote ulimwenguni hapo kesho ambayo ndio Ijumaaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani imeeleza kuwa, Wamarekani na Wazayuni wamefanyia muamala kitu ambacho kimsingi si mali na milki yao.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Palestina ni mali ya Wapalestina na uchukuaji maamuzi kuhusiana na Palestina ni jambo ambalo linapaswa kufanywa na Wapalestina wenyewe na watu wengine hawapaswi kuingilia hilo na kuanza kutoa uamuzi kuhusu ardhi na makazi ya Wapalestina.

Moja ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds nchini Tanzania

Kuitambua rasmi Baitul Muqaddas (Jerusalem) kuwa mji mkuu wa utawala wa Kizayuni, kuupatia utawala huo haramu umiliki wa asilimi 30 ya eneo la Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan, kupingwa haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea nchini kwao na kupokonywa silaha kikamilifu itakayoitwa nchi ya Palestina ni miongoni mwa vipengele vya mpango huo wa udhalilishaji. 

Mpango huo wa kibaguzi umeendelea kulaaniwa katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wea Kiislamu huku kimya cha baadhi ya madola ya Kiarabu kuhusiana na kuporwa haki za Wapalestina nacho kikilaaniwa na wapenda haki kote duniani.

Tags

Maoni