May 23, 2020 02:36 UTC
  • Iran: Marekani kukanyaga sheria zote za kimataifa ndio dhati yake

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu na nusu iliyopita, serikali ya Marekani imekuwa ikikanyaga sheria na maazimio yote ya kimataifa na imekuwa ndiyo dhati yake kutoheshimu kanuni wala sheria na taratibu zinazopaswa kuheshimiwa na kila nchi duniani.

Sayyid Abbas Mousavi alisema hayo jana kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter na huku akiashiria tabia ya kibeberu ya Marekani ya kuendelea kujitoa kwenye mikataba na maazimio ya kimataifa amesema, hatua ya serikali ya Marekani ya kukanyaga sheria zote za kimataifa bila ya shaka itakabiliwa na upinzani mkubwa duniani.

Sayyid Abbas Mousavi

 

Jana Ijumaa, rais wa Marekani, Donald Trump, aliwaambia waandishi wa habari mbele ya Ikulu ya nchi hiyo White House kwamba, nchi yake itajitoa kwenye mkataba wa "Anga iliyo Wazi" baada ya kuituhumu Russia kutoheshimu mkataba huo. Hata hivyo jambo hilo limekuwa ni kitu cha kawaida kabisa kwa Marekani katika kipindi cha miaka mitatu na nusu iliyopita na hadi hivi sasa Trump ameshaitoa Marekani kwenye mikataba mbalimbali ya kimataifa. Kujitoa Marekani kwenye mkataba huo kutakuwa ni pigo jingine kubwa kwa usalama wa nchi za Ulaya.

Wimbi la kujitoa serikali ya Trump katika mikataba na makubaliano ya kimataifa limepelekea kuundika miungano mipya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na siasa za kibeberu za Marekani za kujikumbizia kila kitu upande wake na kutojali maslahi na madhara ya mataifa mengine duniani.

Maoni