May 23, 2020 08:12 UTC
  • Rouhani: Njama za uistikbari wa dunia dhidi ya taifa la Iran zilihitimishwa tarehe 3 Khordad

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuwa siku ya kukombolewa mji wa Khoram-shahr haijasahaulika na kuleza kuwa njama kuu ya uistikbari wa dunia, kimataifa na kieneo dhidi ya taifa la Iran ilihitimishwa tarehe Tatu mwezi Khordad.

Leo Jumamosi tarehe Tatu mwezi Khordad sawa na tarehe 23 Mei siku ya kukumbuka kukombolewa mji wa Khoram-Shahr huko kusini magharibi mwa Iran mnamo mwaka 1982; Siku hii imepewa jina la Siku ya Muqawama, Kujitolea na Ushindi katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Akizungumza leo katika kikao cha Kamati ya Taifa ya Kupambana na Corona Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza maadhimisho ya kukombolewa Khoram-shahr na kuongeza kuwa taifa la Iran katika siku hiyo lilidhihirisha kuwa irada ya wananchi wa Iran ingeibuka na ushindi dhidi ya pande zote hizo hata kama nchi zote pinzani katika eneo na duniani kote zingekuwa bega kwa bega na maadui kupatiwa silaha za kisasa kabisa. 

Raisa Rouhani ameongeza kuwa siku ya kukombolewa Khoram-shahr ni siku muhimu sana katika historia ya taifa, kujitetea kutakatifu na kwa nchi na kwamba furahaya wananchi wa Iran katika kuikomboa Khoram-Shahr haiwezi kusahaulika. 

Harakati za kukombolewa mji wa Khoram-shahr mwaka 1982 

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtoa mkono wa kheri na kupongeza kumalizika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwadia Sikukuu ya Idul-Firt na kueleza kuwa maeneo ya haram mbalimbali yatafunguliwa baada ya Idd kwa kufuatwa kikamilifu protokali za kiafya. 

Tags

Maoni