May 23, 2020 10:15 UTC
  • Wizara ya Ulinzi ya Iran: Tutaendelea kuunga mkono muqawama wa Palestina

Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema itaendelea kuziunga mkono na kuzipa misaada isiyo na kikomo harakati za muqawama za Palestina zinazopambana na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika taarifa ya leo Jumamosi, wizara hiyo imesema: Vikosi vya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu vitaziunga mkono na kuzihami harakati za mapambano haswa kwa kutilia maanani kuwa, ukurasa mpya wa muqawama ulifunguliwa katika harakati za Wapalestina, baada ya Mapinduzi ya Kiislamu, na mlingano wa nguvu daima umekuwa kwa maslahi ya wanamapambano wa Palestina.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku ya kukombolewa mji wa Khoram-Shahr hapa nchini, Wizara ya Ulinzi ya Iran imeeleza bayana kuwa: Njia pekee ya kukabiliana na adui asiye na mantiki na madola ya kiistikbati, ni kutumia lugha ya nguvu na izza.

Leo Jumamosi tarehe Tatu mwezi Khordad sawa na tarehe 23 Mei siku ya kukumbuka kukombolewa mji wa Khoram-Shahr huko kusini magharibi mwa Iran mnamo mwaka 1982; Siku hii imepewa jina la Siku ya Muqawama, Kujitolea na Ushindi katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Baadhi ya makombora ya Iran

Kadhalika Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema itaendelea kujiimarisha na kupiga hatua za maendeleo; sanjari na kuviunga mkono Vikosi vya Ulinzi vya taifa hili, kama sehemu ya kujihami endelevu.

Taarifa ya wizara hiyo imesema taifa hili litaendelea kupata mafanikio katika nyuga mbali mbali kama inavyondelea kushuhudiwa hapa nchini zaidi ya miongo minne licha ya vikwazo.

Tags

Maoni