Jul 02, 2020 06:50 UTC
  • Muhammad Javad Zarif
    Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametangaza kumalizika kikao cha Mchakato wa Astana kilichofanyika kwa njia ya video na kusisitiza kuwa amani itapatikana nchini Syria.

Muhammad Javad Zarif Waziri aliashiria katika ukurasa wake wa Twitter kumalizika kikao cha Marais wa Iran, Russia na Uturuki na kueleza kuwa: Pande hizo zimekubaliana kuendeleza mawasiliano baina ya nchi tatu zinazodhamini mchakato wa Mazungumzo ya Astana na kujikita katika kupunguza hali ya mivutano kupitia mchakato wa kisiasa na kutoa misaada ya kibinadamu.  

Marais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Vladimir Putin wa Russia na mwenzao wa Uturuki, Recep Tayyep Erdogan wamesisitiza katika taarifa yao ya pamoja mwishoni mwa kikao cha jana kilichofanyika kwa njia ya video kwamba: Mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi na kwamba utatatuliwa kupitia mchakato wa kisiasa kati ya Wasyria wenyewe wakisaidiwa na Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama. 

Rais Hassan Rouhani katika kikao cha Mchakato wa Astana kuhusu Syria 

Marais wa Iran, Russia na Uturuki aidha wameeleza azma yao ya kukabiliana na hatua yoyote inayolenga kudhoofisha mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi nzima ya Syria na pia kutishiwa usalama wa taifa wa nchi jirani. 

Maoni