Jul 02, 2020 12:22 UTC
  • Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Ghuba ya Uajemi imeshuhudia jinai za Marekani kwa muda mrefu

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoaa taarifa kwa mnasaba wa kukumbuka jinai ya Marekani ya kutungua kwa makusudi ndege ya abiria ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: "Kwa muda mrefu Ghuba ya Uajemi imekuwa ikishuhudia jinai za Marekani."

Katika ujumbe kupitia Twitter, Wizara ya mambo ya Nje ya Iran imejibu swali kuhusu  maana ya 'Haki za Binadamu za Kimarekani' na kusema: "Haki za binaadamu za Kimarekani maana yake ni kuahidi kufungamana kikamilifu na mauaji ya wanadamu."

Wizara ya mambo ya Nje ya Iran imesema, miaka 32 imepita tokea Marekani iitungue kwa makusudi ndege ya abiria ya Iran na kuongeza kuwa: "Katika tukio hilo watu 290 waliuawa lakini hadi sasa Marekani haijaomba radhi au kubainisha kusikitishwa na kitendo hicho."

Itakumbukwa kuwa siku kama ya leo miaka 32 iliyopita ndege ya abiria aina ya Airbus ya shirika la ndege la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyokuwa ikitoka Bandar Abbas, kusini mwa Iran kuelekea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, ilishambuliwa kwa makombora mawili ya jeshi la Marekani kwenye maji ya Ghuba ya Uajemi. Manowari ya kijeshi ya Marekani USS Vincennes ilifyatua makombora hayo na kuua shahidi watu wote 298 waliokuwa katika ndege hiyo.

Shambulio hilo lilidhihirisha zaidi unyama na ugaidi wa serikali ya Marekani. Viongozi wa Marekani walizidisha ukatili wao pale walipomzawadia medali ya ushujaa nahodha wa meli hiyo kutokana na kitendo hicho kilichotajwa na serikali ya Washington kuwa eti ni cha kishujaa. Miongoni mwa waliouawa shahidi katika hujuma hiyo ya kigaidi ya Marekani walikuwemo watoto 66 na wanawake 53.

Tags

Maoni