Jul 04, 2020 02:40 UTC
  • Ubalozi wa Iran Ufaransa waiambia Saudia: Heshima hainunuliwi kwa pesa za mafuta ya petroli

Ubalozi wa Jamhuri ya Kislamu ya Iran nchini Ufaransa umekosoa na kukemea jinai zinazofanywa na Saudi Arabia na washirika wake nchini Yemen na kusisitiza kuwa: Katika dunia ya sasa hadhi na heshima haviwezi tena kununuliwa kwa fedha za mafuta ya petroli.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Iran nchini Ufaransa katika mtandao wa Twitter imenyesha picha za hali mbaya ya watu wa Yemen, hasara na maafa makubwa yanayosababishwa na mashambulizi ya Saudia na washirika wake dhidi ya taifa hilo na kusema: Kipindi cha kudhamini na kuarifisha usalama kwa kuangalia mguvu za kijeshi peke yake kimepita na kuyoyoma.

Taarifa hiyo iliyokuwa na shaari ya: "Yemen Haiwezi Kupumua" (Yemen Can't Breathe) imeiambia Saudia na washirika wake kwamba: "Dola za mafuta ya petroli haziwezi tena kununua historia, utamaduni, fasihi na ustaarabu."

Wanawake na watoto wa Yemen ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya Saudia.

Wakati huo huo taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Yemen inasema kuwa, zaidi ya Wayemeni laki moja wameuawa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na Saudi Arabia na washirika wake. 

Wizara ya Haki za Binadamu ya Yemen pia imetangaza kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia zimeshambulia mji mkuu wa nchi hiyo, Sanaa na Sa'da huko kaskazini kwa kutumia mabomu yenye nguvu kubwa ya mlipuko ya vishada. Mashambulizi hayo pia yameua wanawake na watoto na kuharibu buhari ilikuwa ya vifaa vya tiba ya Hospitali ya 48 katika eneo la Sab'iin.  

Maoni