Aug 02, 2020 11:28 UTC
  • Rais Rouhani (katikati)
    Rais Rouhani (katikati)

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amebainisha fursa na changamoto za kiuchumi zinazoikabili nchi hiyi na kusema kuwa: Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Iran imepata mafanikio makubwa katika kuzima na kufubaza njama za maadui.

Rais Rouhani ambaye leo alikuwa akihutubia kikao cha Tume ya Serikali ya Uratibu wa Masuala ya Kiuchumi amesema kuwa hali halisi ya uchumi wa nchi inaonesha kuwa, Iran inaweza kuondoka salama katika mbinyo mkubwa unaosababishwa na mashinikizo ya kiwango cha juu wa maadui wake na kushinda vita vya kiuchumi kwa kutumia uwezo wake mkubwa na ushirikiano mzuri baina ya asasi mbalimbali hapa nchini.

Ameashiria ramani ya njia iliyobuniwa katika mpango kabambe wa uchumi na kusema: Lengo kuu la vita vya kiuchumi vya maaduiwa Jamhuri ya Kiislamu ni kuvuruga mipango na usimamizi wa masuala mbalimbali ya nchi.

Rais Rouhani akihutubia kikao cha Tume ya Serikali ya Uratibu wa Masuala ya Kiuchumi

Rais Rouhani amesema kuwa maadui walikuwa wakidhani kuwa baada ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona na taathira za vikwazo haramu na vya kikatili vya maadui hao, uchumi wa Iran utayumbayumba na kutumbukia katika hatari kubwa. 

Ameashiria mafanikio ya asasi mbalimbali za biashara, fedha na idara za serikali katika nyanja mbalimbali na kusema: Mafanikio haya ni matunda ya juhudu kubwa za sekta ya binafsi, wadau wa masuala ya uchumi na usimamizi mzuri wa serikali. 

Tags

Maoni