Aug 13, 2020 13:50 UTC
  • Iran: Pompeo amelihadaa bunge la nchi yake ili kumuuzia silaha mwashamoto wa vita katika eneo

Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amelihadaa bunge la nchi yake ili kuweza kumuuzia silaha mwashaji moto mkuu wa vita katika eneo hili la Asia Magharibi.

Katika taarifa iliyota kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeeleza kuwa: Sasa imeshafichuka na kudhihirika kwamba alichokuwa akihangaikia Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ni kuiuzia silaha nchi ileile ambayo ingali inaendelea kuishambulia kwa mabomu na makombora Yemen, huku akionyesha uzandiki wa kutaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iendelee kuwekewa vizuizi vya slaha.

Katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya jana Jumatano na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Czech mjini Prague, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema: Muamala wa zana za kijeshi ambazo Marekani imeiuzia Saudi Arabia umefanyika kulingana na sheria.

Jinai za kivita zinazofanywa na Saudi Arabia dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Yemen

Pompeo ametoa madai hayo ya kutetea uuzaji silaha kwa Saudia ilhali Mkaguzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameeleza katika ripoti yake kwamba, mnamo mwaka uliopita wa 2019 wakati timu ya Pompeo ilipoongoza mauzo makubwa ya zana za kijeshi na makombora yenye shabaha kali kwa Saudi Arabia haikufanya tathmini kamili kuhusu hatari ya maafa watakayopata raia wa Yemen kutokana na hujuma za silaha hizo.../

Tags

Maoni