Aug 14, 2020 07:57 UTC
  • Ujumbe wa Zarif katika kumbukumbu ya ushindi wa Hizbullah katika Vita vya Siku 33

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe wa pongezi kwa kwa serikali na watu wa Lebanon kwa mnasaba wa mwaka wa 14 wa ushindi uliojaa fahari wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika Vita vya Siku 33.

Mohammad Javad Zarif ametuma salamu kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon na kuwapongeza kwa mnasaba wa mwaka wa 14 wa ushindi uliojaa fahari wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika Vita vya Siku 33. 

Siku kama ya leo miaka 14 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 14 Agosti 2006, yalimalizika mapigano kati ya harakati ya Hizbullah ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya kutolewa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikubaliwa na pande hizo mbili. Mapigano hayo yalimalizika kwa ushindi wa Hizbullah na utawala wa Kizayuni wa Israel ulilazimika kurudu nyuma baada ya kupata hasara kubwa.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah

Mohammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Alhamisi aliwasili mjini Beirut, Lebanon kwa lengo la kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo kuhusu misaada ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Lebanon pamoja na masuala mengine. 

Tags

Maoni