Sep 12, 2020 11:33 UTC
  • Rouhani: White House haifahamu chochote kuhusu ubinadamu

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Ikulu ya White House ya Marekani haina ufahamu wowote kuhusu utu na ubinadamu.

Rais Rouhani amesema hayo mapema leo katika kikao cha Jopokazi la Kitaifa la Kupambana na Kuzuia Corona ambapo ameikosoa vikali Washington kwa kuzuia taifa la Iran lisifikiwe na hata dawa katika kipindi cha janga la virusi vya corona.

Amefafanua kuwa: Tuliiomba IMF mkopo wa dola bilioni 5 ambapo wanachama wote walikubali ombi letu, lakini Marekani ilikataa tupewe mkopo huo ambao ungelisaidia katika kununua dawa, uzalishaji wa chanjo, na kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Iran. (Wamarekani) Wapo mbali na ubinadamu kiasi hiki.

Dakta Rouhani ameeleza bayana kuwa, Marekani imeenda mbali zaidi na hata kuzitishia nchi rafiki za Jamhuri ya Kiislamu ili ziendelee kuzuilia fedha za Iran zilizo katika benki za nchi hizo.

Rais wa Iran amebainisha kuwa, Wamarekani wanahamakishwa na hali ya maisha kuwa ya kawaida hapa nchini licha ya janga la corona na mashinikizo ya kiwango cha juu ya watawala wa Washington dhidi ya taifa hili.

Rais Rouhani ameashiria kuhusu ripoti mbili alizopokea kutoka Wizara ya Intelijensia juu ya ripoti mbili za taasisi za Marekani zinazoonyesha kuwa Wamarekani waliingiwa na kiwewe kutokana na maisha na biashara kuendelea kama kawaida hapa nchini licha ya corona na kusema kuwa: Taasisi hizo zimesema Marekani ilishadidisha mashinikizo yake dhidi ya Iran ili kuibuke ghasia za uasi, kutokana na masaibu ya corona hapa nchini, lakini hilo halikufanyika. 

Tags

Maoni