Sep 19, 2020 12:56 UTC
  • Mava Scott
    Mava Scott

Idara ya Usalama wa Taifa ya Afrika Kusini imesema hakuna ushahidi wowote iliyoupata wa madai ya Marekani kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapanga kumuua Lana Marks, Balozi wa Marekani katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Mava Scott, msemaji wa Wakala wa Kitaifa wa Usalama wa Afrika Kusini amesema taarifa waliyopokea haitoshi kuyapa nguvu madai ya kuwepo tishio kwa usalama wa Balozi wa Marekani nchini.

Ameeleza bayana kuwa, "njama za mauaji dhidi ya wanadiplomasia ni jambo linalochukuliwa kwa uzito mkubwa. Tumemhakikishia Mheshimwa Balozi Marks juu ya kujitolea kwetu katika suala hili."

Idara ya Usalama wa Taifa ya Afrika Kusini imetaka Marekani iwasilishe taarifa zaidi juu ya madai yake, huku ikizitaka pande husika katika kadhia hii kuwa na utulivu.

Marais wa Iran na Afrika Kusini. Kuimarika uhusiano wa Iran na Afrika Kusini licha ya njama za maadui

Katika mahojiano na Shirika la Taifa la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC News) siku ya Alkhamisi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini Dakta Naledi Pandor alisema kuwa, taifa hilo limestaajabishwa na madai hayo ya Marekani dhidi ya Iran. Alihoji kwa kusema, "Inawezekanaje Iran, rafiki mkubwa wa Afrika Kusini ije hapa nchini na kufanya kitendo kiovu kama hicho katika nchi ambayo pia rafiki yake?"

Jamhuri ya Kiislamu imesema madai kuwa nchi hii inapanga kumuua mwanadiplomasia huyo wa Marekani eti kama kisasi cha mauaji ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ambaye aliuawa shahidi mapema mwaka huu katika shambulizi la kigaidi la jeshi katili Marekani nchini Iraq, ni muendelezo wa Marekani kutumia mbinu chafu za kukaririwa kwa shabaha ya kueneza proganda chafu dhidi ya Iran katika uga wa kimataifa.

Tags

Maoni