Sep 22, 2020 02:35 UTC
  • Grossi apongeza mapatano yaliyofikiwa kati ya wakala wa IAEA na Iran

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) kwa mara nyingine tena amepongeza mapatano yaliyofikiwa baina ya wakala huo na Jamhuri ya Kiislamu Iran.

Rafael Grossi jana Jumatatu alieleza kuwa, anataraji kwamba mapatano hayo kati ya Iran na wakala wa IAEA yataimarisha ushirikiano wa pande mbili. Grossi aliyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha 64 cha Mkutano Mkuu wa Wakala wa IAEA mjini Vienna huko Austria.

Grossi alisema kuwa: Wakala wa IAEA utaendelea kukaguzi miradi ya nyuklia ya Tehran kwa mujibu wa mapatano ya masuala ya usalama. Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia aliongeza kusema kuwa: Taasisi hiyo ya kimataifa itakuwa ikitoa ripoti kwa Bodi ya Magavana ya IAEA kuhusu utekelezaji wa majukumu ya kinyuklia wa Iran kwa mujibu wa mapatano ya JCPOA. 

Kikao cha 64 cha Mkutano Mkuu wa wakala wa IAEA kinaendelea na shughuli zake huko Vienna hadi Ijumaa wiki hii kwa kikihudhuriwa na mabalozi na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi 171 wanachama wa IAEA na kwa njia ya video.    

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia tarehe 26 mwezi Agosti mwaka huu zilitoa taarifa ya pamoja mwishoni mwa safari ya siku mbili ya Rafael Grossi hapa Tehran. 

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Rafael Grossi (kulia) katika mazungumzo hapa Tehran na Ali AKbar Salehi, Mkuu wa Taasisi ya Nyuklia ya Iran

 

Tags

Maoni