Sep 23, 2020 13:26 UTC
  • Rouhani: tuhuma na mahesabu ghalati ya Saddam zinakaririwa leo na Marekani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria vita vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: tuhuma na mahesabu ghalati ya viongozi wa White House yanafanana na hatua zilizochukuliwa na utawala wa Saddam na kupelekea kuangamizwa utawala huo.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesema leo katika kikao cha baraza lake la mawaziri kwamba: uwongo na mahesabu ghalati ni sababu kuu iliyoupelekea utawala wa Saddam kuishambulia Iran na kusisitiza kuwa: Saddam alifedheheshwa na tuhuma na mahesabu hayo potofu na kujiangamiza mwenyewe; na hata waungaji wake mkono wa kieneo mmoja baada ya mwingine walieleza kujutia vitendo vyao hvyo vya kumuunga mkono na kumsaidia Saddam.  

Saddam Hussein, dikteta wa zamani wa Iraq aliyeng'olewa madarakani   

Rais Rouhani amesema kuwa, leo hii pia viongozi wa White House wanakariri tuhuma kama hizo, na serikali ya Marekani miaka miwili iliyopita ilianzisha vita vya kiuchumi vya pande zote kwa kutoa tuhuma na kutekeleza mahesabu ghalati; ambapo matokeo ya hatua hizo yamebainika wazi kikamilifu.   

Rais wa Iran ameashiria kushindwa Marekani mbele ya Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa: Hii leo ule ukubwa wa Marekani na ushawishi iliokuwua ikidhani inao duniani umeporomoka. 

Rais Rouhani amesema kuwa, taifa la Iran lilisimama imara katika vita vya miaka 8 vya Kujitetea Kutakatifu na kupata ushindi mkubwa wa kihistoria kwa upande wa  kijeshi na kiulinzi. Amesema, leo hii pia taifa la Iran limepata mafanikio makubwa kisiasa, kisheria na kidiplomasia.   

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: kujiamini na kusimama imara wananchi ni sababu ya ushindi wa jana na wa leo wa taifa la Iran na kwamba Jamhuri ya Kiislamu haijawahi kuanzisha vita dhidi ya yoyote na kwamba wananchi wa Iran watavishinda pia vita hivi vya kiuchumi kwa muqawama na kupambana kiume. 

Tags

Maoni