Sep 24, 2020 12:03 UTC
  • Brigedia Jenerali Dehqan: Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalitoa pigo la kihistoria dhidi ya Marekani

Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi amesema kuwa, ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa pigo kubwa zaidi la kihistoria dhidi ya Marekani na yaliinasua nchi hii kutoka katika makucha ya ukoloni wa Magharibi.

Brigedia Jenerali Hossein Dehqan amesema hayo leo mjini Hamedan magharibi mwa Iran na kueleza kwamba, baada ya taifa la Iran kuishinda kambi ya ukafiri lilitangaza kuwa, uwepo wa Marekani katika eneo ni kinyume cha sheria na kwamba, kuutetea na kuuhami utawala vamizi wa Israel ni ni harmu na jambo lisilofaa.

Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi  amebainisha kwamba, Marekani ilikuwa ikiamini kuwa kujitoa kwake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na wakati huo huo kutekeleza mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa ingeweza kusambaratisha mfumo wa uchumi wa Iran katika kipindi cha chini ya miezi mitatu na baada ya hapo ingezusha vurugu na machafuko na hivyo kuusambaratisha mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini.

Brigedia Jenerali Hossein Dehqan, Mshauri wa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Iran katika masuala ya sekta ya viwanda vya ulinzi 

 

Brigedia Jenerali Dehqan aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, licha ya Marekani kupata ibra na mafunzo makubwa kupitia mambo mbalimbali iliyofanya, lakini pamoja na hayo kuna uwezekano ikachukua maamuzi kwa kutegemea mahesabu yasiyo sahihi na kuanzisha kambi mpya dhidi ya Iran, hatua ambayo nayo itakabiliwa na jibu litakaloifanya ijute.

Tags

Maoni