Oct 07, 2020 04:47 UTC
  • Iran yazindua kizazi kipya cha mfumo wa rada wa Qadir

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limezindua kizazi kipya cha mfumo wa rada wa ulinzi wa anga uliopewa jina la Qadir ambao ni wa masafa marefu na unaotumia mfumo wa 3D.

Akihutubia katika hafla ya uzundizi wa mfumo huo jana Jumanne katika mkoa wa Yazd katikati mwa Iran, Kamanda wa Kikosi cha Anga za Mbali cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Brigedia Jenerali Amir-Ali Hajizadeh amesema Iran ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza duniani kwa uundaji wa mifumo ya rada. 

Amesema mifumo miwili ya rada iliyozinduliwa ina uwezo wa kugundua vyombo vinavyoruka angani hadi umbali wa kilomita 350, na uwezo huo unaweza kuongezeka hadi kilomita 1,000 kwa kutegemea umbali wa kifaa kinachofuatiliwa.

Brigedia Jenerali Amir-Ali Hajizadeh ameeleza bayana kuwa, iwapo kuna makampuni 20 ya kuzalisha mifumo ya rada ya ulinzi wa anga duniani, basi Jamhuri ya Kiislamu ni katika nchi 10 bora kwa uzalishaji wa mifumo hiyo.

Brigedia Jenerali Amir-Ali Hajizadeh

Mfumo wa rada wa Qadir ulioundwa na wataalamu wa Iran ulizinduliwa mara ya kwanza hapa nchini mwaka 2013 na jeshi la IRGC, na tayari vizazi vinane vya mfumo huo vimewashawekwa katika kona mbalimbali za nchi.

Licha ya kukabiliwa na vikwazo pamoja na mashinikizo ya madola ya Magharibi, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata mafanikio makubwa mno katika sekta ya ulinzi kwa kuweza kujitegemea na kujitosheleza katika uundaji silaha na zana za kijeshi.

Tags

Maoni