Oct 19, 2020 03:04 UTC
  • Rouhani: Iran imefelisha njama za Marekani la kuisambaratisha nchi

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maadui wa Iran walikuwa na mpango maalumu wa kuzusha mifarakano na migongano humu nchnii ili viwazo vyao vipate nguvu zaidi.

Akizungumza jana Jumapili, Rais Rouhani ametoa wito kwa maafisa wote wa serikali, wanaharakati na wote wanaoupenda mfumo wa Kiislamu na nchi yao wajiepushe na mizozo na mifarakano huku wakidumisha utulivu wa kisiasa na kutumia busara.

Huku akiashiria mpango wa serikali wa kukabiliana na vita vya kiuchumi vya Marekani Rais Rouhani amesema: "Ingawa vikwazo vya Marekani ambavyo ni kinyume cha sheria na ni dhidi ya ubinadamu vimepunguza pato la fedha za kigeni la Iran, lakini sasa baada ya miaka 2.5 ya vikwazo hivyo, serikali imefanikiwa kuizuia Marekani kufikia lengo lake chafu la kuisambaratisha Iran."

Rais Rouhani amesisitizia ulazima wa kudumisha utulivu wa kisiasa na maelewano nchini na kuongeza kuwa: "Mbali na kuwekeza katika vikwazo vya kiuchumi, maadui pia wamewekeza sana katika kuibua mifarakano na ghasia ndani ya nchi ili vikwazo vyao vifanikiwe."

Rais Rouhani amesema serikali inaitazama sekta binafsi kama nguvu yenye kuusukuma mbele uchumi na kuongeza kuwa uungaji mkono kwa sekta binafsi ni kati ya sera muhimu za kiuchumi za serikali yake. 

Tags

Maoni