Oct 20, 2020 02:35 UTC
  • Brigedia Jenerali Amir Hatami
    Brigedia Jenerali Amir Hatami

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kusaini mikataba ya masuala ya kijeshi na usalama na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi.

Brigedia Jenerali Amir Hatami ametoa sisitizo hilo katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na televisheni ya Aljazeera. 

Amesema, kuna makubaliano ambayo Iran imesaini na Russia na China baada ya kumalizika marufuku ya kuuza na kununua silaha iliyokuwa imewekewa na akaongeza kuwa, Iran imefikia makubaliano muhimu na Russia kuhusiana na kupanua na kustawisha mifumo ya vikosi vya anga.

Brigedia Jenerali Hatami ameeleza kwamba, kumalizika marufuku ya silaha iliyokuwa imewekewa Iran kunatoa fursa ya kukidhi mahitaji ya silaha na kuuza zana hizo za kijeshi kwa nchi zingine.

Image Caption

Katika mahojiano hayo, Waziri wa Ulinzi wa Iran amezungumzia pia hatua ya Imarati na Bahrain ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel na akaeleza kwamba, hatua hiyo ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi. Ameonya kuwa, kitisho chochote kitakachofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo hili kitakabiliwa na jibu la wazi na la moja kwa moja.

Brigedia Jenerali Amir Hatami amesisitiza pia kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitafanya mazungumzo yoyote ya Marekani kuhusiana na mfumo wake ulinzi wa makombora na wala hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuitaka Tehran ifanye hivyo.../

Tags

Maoni