Oct 24, 2020 04:20 UTC
  • Wademokrat wa Seneti ya Marekani wapinga madai ya Trump dhidi ya Iran

Mwenyekiti wa Wademokrat katika Seneti ya Marekani na vilevile Spika wa Kongresi ya nchi hiyo wamepinga madai yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Tasisi ya Usalama wa Taifa kwamba Iran inaingilia uchaguzi wa rais wa Marekani.

Spika wa Kongresi ya Marekani kutoka chama cha Democratic, Nancy Pelosi ameashiria kikao cha mwongozo kilichofanyika na maafisa wa vyombo vya upelelezi vya nchi hiyo na kupinga madai ya maafisa hao kwamba Iran inaingilia uchaguzi wa rais wa Marekani. 

Vilevile gazeti la The Hill la Marekani limeripoti kuwa, mwenyekiti wa Wademokrat waliowachache katika Bunge la Seneti, Charles Schumer amesema kuwa, taarifa za siri zizotolewa na Mkurugenzi wa Taasisi za Usalama wa Taifa, John Ratcliffe katika kikao cha Kongresi Jumatano iliyopita zinaonyesha kuwa Iran haina mpango wa kutoa pigo kwa Donald Trump. 

John Ratcliffe amedai kuwa Iran na Russia zinakula njama ya kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani.

John Ratcliffe

Wakati huo huo balozi wa Uswisi nchini Iran ambaye ndiye anayelinda maslahi ya Marekani hapa nchini ameitwa kusailiwa katika Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Iran baada ya kutolewa madai hayo ya serikali ya Washington.  

Awali Msemaji wa Ofisi ya Iran katika Umoja wa Mataifa alipuuzilia mbali madai kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaingilia uchaguzi wa Marekani na kusema: "Kinyume na ilivyo Marekani, Iran haingilii chaguzi za nchi nyinginezo duniani."

 Alireza Miryousefi amesema dunia imekuwa ikishuhudia namna hata maafisa wa ngazi za juu wa Washington wanavyotilia shaka matokeo ya uchaguzi wao wenyewe.

Tags