Oct 28, 2020 07:45 UTC
  • Iran: Njama mpya za Marekani na Israel dhidi yetu zitafeli

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema njama mpya za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kutoa pigo kwa Iran kupitia uanzishwaji wa uhusiano wa kawaida na Tel Aviv, zitagonga mwamba.

Mohsen Rezaei amesema hayo akihutubia Kongamano la Kimataifa kuhusu kuangamia Marekani, lililofanyika jana Jumanne katika jengo lililokuwa la ubalozi wa Marekani hapa jijini Tehran na kuongeza kuwa, 'bila shaka njama mpya iliyoanzishwa na Marekani na Israel ya eti kuwaunganisha Waarabu na Israel dhidi ya Iran itafeli."

Siku chache zilizopita, Marekani ilitangaza kuwa Sudan imeamua kufuata mkumbo wa Imarati na Bahrain wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel. Sudan inakuwa nchi ya tatu ya Kiarabu baada ya Imarati na Bahrain kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, licha ya pingamizi na malalamiko ya wananchi wa mataifa hayo ya Kiarabu.

Rezaei amekumbusha kuwa, kuporomoka kwa serikali ya Marekani ni suala lenye umuhimu mkubwa, na kwamba Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ulilipa eneo la Asia Magharibi na dunia nzima kwa ujumla mwamko na mawazo mapya ya kupambana na ustaarabu na utamaduni wa Marekani na Magharibi.

Kuporomoka zaidi uchumi wa Marekani kutokana na janga la corona

Katibu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa, uchumi wa Marekani ambayo ni nguzo ya uwezo wa Washington umedorora na hivi sasa dola hilo la kibeberu haliwezi tena kuzifadhili serikali dhalimu katika maeno mbalimbali duniani.

Ayatullah Larijani amebainisha kuwa, Marekani imepoteza dira na uwezo wake katika sehemu tofauti za dunia, na mbinu mbadala inazotumia kama vita dhidi ya Yemen vinavyoongozwa na Saudia zimefeli pia.

Tags

Maoni