Oct 29, 2020 08:12 UTC
  • Iran kuvigeuza vikwazo vipya dhidi yake kuwa waraka usio na itibari

Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa hili litavigeuza vikwazo vipya lilivyowekewa na Marekani kuwa waraka usio na itibari.

Mahmoud Vaezi amesema hayo katika ujumbe wake wa Twitter na kuongeza kuwa, uraibu wa vikwazo wa timu ya Ikulu ya White House ya Marekani unaonyesha namna watu waliomzunguka Rais Donald Trump walivyokata tamaa.

Amesema uraibu wa vikwazo unaonyesha namna sera za hivi sasa za Marekani zimefeli na kugonga mwamba.

Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza bayana kuwa: Taifa hili litavigeuza vikwazo vipya lilivyowekewa na Marekani kuwa waraka usio na itibari wa Wamarekani wenye misimamo mikali.

Uraibu wa vikwazo wa US

Usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii, Wizara ya Hazina ya Taifa ya Marekani ilitangaza vikwazo vipya dhidi ya Wizara ya Mafuta ya Petroli ya Iran, mashirika yanayofungamana nayo na Waziri wa Mafuta wa Iran, Bijan Namdar Zanganeh, pamoja na maafisa wengine wa wizara hiyo.

Marekani imeshindwa kufikia malengo yake ya kutaka kuipigisha magoti Jamhuri ya Kiislamu kwa kuiwekea vikwazo vya kiwango cha juu kabisa ambavyo havijawahi kuwekewa nchi yoyote ile, na hivi saa inavitumia vikwazo hivyo kama wenzo za kufanya kampeni za uchaguzi mkuu wa Novemba 3.

Tags

Maoni