Oct 29, 2020 11:22 UTC
  • Ayatullah Ali Khamenei
    Ayatullah Ali Khamenei

Kingozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amewatumia ujumbe vijana wa Ufaransa akiwataka wamhoji Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron kwa nini kwa nini anamtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa jina la uhuru wa maoni?

Katika ujumbe huo uliotumwa jana usiku kwa vijana wa Ufaransa, Ayatullah Khamenei amesema: Je, uhuru wa kujieleza una maana ya matusi, haswa kuwatukana watu watukufu? Je, kitendo hiki cha kijinga si dharau na kejeli kwa hisia za taifa lililomchagua kuwa rais wake? 

Katika swali jingine Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amehoji kwamba: Kwa nini kutilia shaka Holocaust (mauaji yanayodaiwa kufanywa na Manazi) dhidi ya Wayahudi kunatambuliwa kuwa ni kosa la jinai? Kwa nini anayeandika lolote kudadisi mauaji hayo (ya Holocaust) anafungwa jela, lakini kumtusi Mtume Mtukufu SAW kunaruhusiwa na kukuaririwa nchini Ufaransa kwa kutumia jina la uhuru wa kuejieleza na kusema?

Baadhi ya nchi za Magharibi ikiwemo Ufaransa zimekuwa zikipeleka mbele siasa na maslahi yao kwa kutumia kisingizio cha demokrasia na uhuru wa kujieleza. Wamagharibi hao hususan huko Ufaransa sasa wanafanya hujuma dhidi ya Uislamu na Waislamu ilhali dini hiyo inatambuliwa kuwa dini ya huruma, upendo na amani. Mtume Muhammad (saw) ambaye hivi sasa tunasherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, ndiye nguzo ya umoja na mshikamano baina ya Waislamu kote duniani na anaheshimiwa na dini zote za mbinguni. Hii ni pamoja na kuwa, kuheshimu dini za mbinguni ni msingi wa upendo, amani na hali ya kuaminiana baina ya wanadamu.

Kuchupa mipaka kunalaaniwa katika dini na madhehebu yote, lakini suala hilo halipaswi kutumiwa na viongozi wa Ufaransa kwa ajili ya kuhudumia maslahi yao ya kisiasa. Hivyo, matusi na dharau ya Rais wa Ufaransa dhidi ya Mtume Muhammad (saw) kwa kutumia kisingizio cha uhuru wa kusema na kujieleza, haiwezi kutetewa kwa njia yoyote wala hayasaidii kuleta amani na maelewano baina ya wafuasi wa dini tofauti. 

Kadinali Mar Lois Rafael Sako wa Kanisa Katoliki la Kaldani nchini Iraq (Chaldean Catholic Church) Jumatano ya jana alitoa taarifa akisema kuwa: "Dini zote zinapaswa kuwa chanzo cha upendo, amani na ushirikiano na kujenga hali ya kuaminiana baina ya watu, na si kueneza chuki na uhasama."

Mienendo ya Rais wa Ufaransa dhidi ya Waislamu haiwezi kutetewa na dini yoyote ile; na kinyume chake, inasababisha wasiwasi katika jamii ya kimataifa. Misimamo ya kindumakuwili ya rais huyo wa Ufaransa katika kutumia vibaya uhuru wa kujieleza ni dharau na kulivunjia heshima taifa lililompigia kura; kwa sababu uhuru wa kujieleza hauna maana ya kuvunjia heshima dini na itikadi za watu wengine.

Nukta ya kutiliwa maanani ni kwamba, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya ametetea kitendo cha jarida la Charlie Hebdo cha kuchapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) licha ya kwamba, sheria ya Ufaransa inamhukumu kifungo mtu yeyote anayetilia shaka au kuhoji baadhi ya mambo kama kuhoji idadi ya Mayahudi walioliwa katika vita vya Pili vya Dunia (Holocaust).

Mienendo hii ya kindumakuwili ya nchi za Magharibi hususan Ufaransa ndiyo stratijia kuu inayotawala sera na siasa za nchi nyingi za Magharibi kuhusiana na Uislamu.       

Tags