Oct 29, 2020 12:18 UTC
  • Spika Qalibaf: Kuanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel hakutadumu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewahutubu baadhi ya watawala wa nchi za Kiislamu ambao wameanzisha uhusiano wa kawaiada na utawala haramu wa Israel na kusema kuwa, viongozi wa mataifa hayo wanapasa kutambua kwamba, hilo halitadumu lakini doa baya katika historia litabakia kwa jina lao mbele ya wananchi wa mataifa ya Kiislamu na watu huru duniani.

Muhammad Baqir Qalibaf amesema hayo leo katika hafla ya ufumnguzi wa Mkutano wa 34 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu hapa mjini Tehran na kubainisha kwamba, mambo ya pamoja ya Umma wa Kiislamu ni mengi mno kiasi kwamba, hakuna kisingizio chochote kinachobakia cha mifarakano na mivutano.

Spika wa Bunge la Iran amesema, Quds ni kibla cha kwanza cha Waislamu na moja ya mambo ya kuwaunganisha pamoja Waislamu.

Quds

 

Qalibaf amesema pia kuwa, Palestina itaendelea kuwa kadhia ya kwanza katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, kuunga mkono malengo matukufu ya Palestina na Quds Tukufu ni jambo linaloleta mfungamano baina ya Waislamu.

Spika Qalibaf ameitaja Wiki ya Umoja kama nembo ya mshikamano wa Umma wa Kiislamu na kwamba, umoja na udugu wa Kiislamu ni moja ya misingi muhimu ya Uislamu.

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ameashiria katika hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa kimataifa wa Umoja wa Kiislamu kuhusu vitendo vya kuvunjiwa heshima Bwana Mtume SAW huko nchini Ufaransa na kusema kuwa, kitendo chochote cha kumvunjia heshima Mtume SAW maana yake ni kuwavunjia heshima Mitume wote na vitabu vya mbinguni.

Tags

Maoni